Maafisa wa polisi eneo la kesses wamewatia mbaroni watu wanne akiwemo meneja moja wa benki moja , afisa mmoja wa polisi na mumiliki wa baa moja maarufu eneo la cheptret waliopatikana wamejifungia katika chumba cha kulala wakibugia pombe.
Wananchi eneo la cheptiret waliwawafahamisha maafisa wa polisi kuhusu baa ya eldorant ambayo inasemekana imekuwa ikutumiwa na watu wanaosafiri kutoka jijini Nairobi ili kuendeleza unywaji pombe kinyume na maagizo ya serikali na wizara ya afya.
Wanne hao wamelazimishwa kusalia katika karantini ya lazima ya siku 14 eneo la kamalel.
Kamishana wa kaunti ya uasingishu abdulzack jaldesa amesema kuwa sheria lazima itafuatwa haswa kwa wale watakaokiuka masharti yaliyowerkwa wakati huu wa maanbukizi ya virusi vya corona.