baadhi ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kaunti ya uasigishu wamemkashifu vikali gavana jackson ma ndago aliyetoa matamshi kwamba wazee wa umri huo hawaruhisiwi kutoka kwenye nyumba zao ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
wazee hao wamesema ugonjwa huo hauchagui umri na kwamba unaweza kumpata mtu yeyote. wakizungumza mjini eldoret wameshangaa iwapo gavana huyo ataweza kutoa chakula kwa hao wote huku badhi yao wakishikilia kwamba wanategemewa na familia zao na kwamba wataendelea kufanya shughuli zao njini eldoret.