Papa Fransisco aanzisha Mchango wa Kuwasaidia Waathiriwa wa Covid-19

Papa Mtakatifu Francisko ameanzisha Mfuko wa Dharura ili kusaidia juhudi za Makanisa mahalia kupambana na athari za Virusi vya Corona, COVID-19.

Papa amechangia kiasi cha dola 750, 000 kama kianzio na anawaalika watu wa Mungu kuchangia katika Mfuko wa Dharura kupitia kwenye Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa katika nchi zao.

Hiki ni kielelezo cha huruma na ukarimu unaojenga na kudumisha umoja na mshikamano na Makanisa mahalia katika kipindi hiki kigumu na chenye changamoto pevu katika maisha na utume wa Kanisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *