Mapadre waadhimisha Misa bila Wakristu

Ikiwa ni jumapili ya mwisho kabla ya pasaka,wakristo wanazidi kuhimizwa kushiriki sherehe hii wakiwa nyumbani.

Tofauti na miaka zilizopita,wakatoliki hawaja kongamana na kuandamana kama ilivyo desturi kwani sharia zilizowekwa kukabili maambukizi ya covid-19  ziliwabana  kutekeleza maandamano hayo.

Katika kanisa la moyo mtakatifu wa yesu cathedral,misa iliandaliwa kwa mapadre 5 kwa niaba ya wakristu  na iliongozwa na padre mkuu William Kosgey  huku wakizingatia umbali wa mita moja unusu,kama ishara ya tamaduni hii.

Kinyume na miaka zilizopita,ambapo maelfu ya watu hukusanyika kwa sherehe hii,ni mapadre 6 kwa jumla tu ambao waliruhusiwa kushiriki maandamano ya mitende kanisani huku wakristu wakiimizwa kufuata misa hiyo kwa mitandao ya kijamii ikiwemo stesheni ya Upendo Fm.

Uamuzi huu ulitekelezwa baada ya kupewa idhini kutoka kwa kamishna wa kaunti ya Uasin gishu bw.Abdirizak Jaldesa. Mapadre kutoka parokia mbalimbali pia walibuni mbinu ya kuwashirikisha wakristu katika sherehe ya mitende ikiwemo kutumia mitandao ya kijamii kama facebook,youtube miongoni mwa zingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *