Wetangula; Mfanyieni Majaribio Ya Covid-19 Kwingine

Seneta wa Bungoma Moses Wetangu’la amepinga wazo la baadhi ya mataifa ya Ulaya na wanasayansi kutaka majaribio ya chanjo ya COVID-19 kufanywa kwa kuwatumia Waafrika.

Hii ni baada ya madaktari Ufaransa kupendekeza kuwa itakuwa ni bora hivyo kwa kudai kuwa Afrika “haina uwezo wa kukabiliana na COVID-19”.

Katika ujumbe wake wenye kauli nzito, seneta huyo wa Bungoma ambaye pia ni kiongozi wa chama cha FORD Kenya aliwataka viongozi Afrika kukataa wazo la aina hiyo kwa kusema Waafrika si “Panya”.

Wazo hilo lilikuwa limegusa wengi mishipa barani Afrika na duniani na liliwafanya Wakenya kuingia mitandaoni kumwaga kauli zao na kukashifu mataifa ya Ulaya na wanasayansi kwa kuwaona Waafrika kama “panga wa majaribio”.

Ulimwenguni kote kuna visa zaidi ya 1 milioni vya COVID-19 na tayari zaidi ya vifo 59, 172 vimeripotiwa.

Katika idadi hiyo, Marekani ina idadi kubwa ya visa vya maambukizi na kufikia sasa ina zaidi ya 277,460 na ni ya tatu katika vifo – 7, 402.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *