Askofu Mkuu Anyolo: Tushirikiane tushinde Changamoto za Maisha

Waumini wa kanisa katoliki  kote duniani wameadhimisha Jumapili ya Mitende, hii leo, huku sherehe ya pasaka ikitarajiwa kufanyika wiki ijayo, ikiwa ni ukumbusho wa kifo na ufufuo wa Yesu kristo.

Askofu mkuu Philip Anyolo wa jimbo kuu la Kisumu  ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la maaskofu nchini,KCCB,ameongoza ibada misa ya jumapili ya mitende katika kanisa la Holy Basilica jijini Nairobi.

Misa hiyo ilihudhuriwa na kadinali John Njue miongoni mwa mapadre wasozidi kumi. Askofu mkuu amehimiza wakristu kuombea afya haswa wakati huu ambapo dunia inapigana na maambukizi ya virusi vya corona. Askofu mkuu amehimiza unyenyekevu na utii kwa wakristu huku wakifuata mfano wa Yesu.

Askofu amewaomba wakristu kushirikiana na kuwa jamaa moja ili kuweza kupigana na changamoto katika maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *