Papa Francisko: Kimbilieni huruma ya Mungu

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake kuhusu Heri za Mlimani, amegusia kuhusu alama za kifo zinazomzunguka mwanadamu katika ulimwengu mamboleo.

Watu wanaishi katika hofu na taharuki kubwa! Katika muktadha huu, Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumkimbilia Kristo Yesu kwa kutambua kwamba, hawako peke yao.

Kwa hakika Yesu, atawasindikiza na kuwaongoza kwa sababu kamwe hawezi kumdanganya mtu. Katika kipindi hiki kigumu cha wasi wasi na hofu ya maambukizi makubwa ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona, COVID, Baba Mtakatifu anawataka waamini kukimbilia Huruma ya Mungu kwa njia ya maombezi ya Mtakatifu Yohane Paulo II, Mama Kanisa anapoadhimisha kumbu kumbu ya Miaka 15 tangu alipofariki dunia, hapo tarehe 2 Aprili 2005. Amewataka waamini kujiandaa vyema katika maadhimisho ya Fumbo la Pasaka, ili kila mmoja wao, aweze kuonja uwepo endelevu wa Kristo Yesu katika hija ya maisha yake ya kila siku!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *