Rais uhuru Kenyatta pamoja na waziri wa afya Mutahi Kagwe wamewasifia waathiriwa wa kwanza wawili waliopona maabukizi ya virusi vya corona kuwa kupitia mawasiliano ya moja kwa moja ya video.
Rais Kenyatta amesema kuwa wawili hao ni wenye ujasiri na kuigwa mfano kwa wakenya wengine kama wazalendo na wanaojali wengine.
Mazungumzo hayo yameangazia huduma za kiafya pamoja na mikakati ambayo serikali imeweka katika kupambana na virusi hivyo hatari.
Waathiriwa hao ambao ni Brenda na brian ni miongoni mwa waathiriwa wa kwanza wa virusi vya corona wamewaeleza wakenya kutoogopa janga hili ila tu wazingatie usafi na mikakati iliyowekwa na serikali na bila shaka wataishinda vita hivyo.