Baada ya taifa la Kenya kusaijili visa 81 vya maambukizi ya virusi vya corona inayopelekea ugonjwa wa Covid 19 hio jana ni rasmi kuwa visa vya maambukizi hayo yanasambaa kwa idadi ya juu kwa sasa.
Akizungumza na vyombo vya habari waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe hata hivyo amesema kwamba kuna habari njema baada ya wagonjwa watatu kuripotiwa kupona.
Mutahi Kagwe amesema kwamba wagonjwa 13 ni wanaume na tisa ni wanawake. Wagonjwa hao wanashirikisha Wakenya 18, raia 2 wa Pakistan na raia 2 wa Cameroon.
Idadi ya maambukizi, waliopona na hata vifo zinazidi kusajiliwa humu nchini, ukanda wa afrika mashariki, barani afrika na ulimwenguni kote.
Kufikia sasa taifa la Rwanda linaongoza katika ukanda wa afrika mashariki huku ikisajili visa 82, Kenya 81, Uganda 44, Ethopia 29, Tanzania 20, Somalia 5, Burundi 2, huku Sudan ya kusini ikiwa haijaandikisha kisa chochote kufikia sasa.
Maeneo mengine ya barani afrika ni kuwa Afrika ya kusini ina visa 1380, Misri visa 779, Nigeria 174, Congo visa 22.
Ulimwenguni marekani inaongoza jedwali kwa visa vingi duniani 215, 215 huku ikisajili vifo 5, 110, Italia inafuata kwa ukaribu 110, 574 huku ikisajili vifo 13, 155.
Uhispania ina 104, 118 huku ikiwa na visa 9, 387. Kwa sasa dunia imesajili visa 936, 204 huku kukiwa na vifo 47, 249 na wale waliopona wakiwa ni 194, 578