Misa ya kwanza ya Askofu Kimengich

Askofu mpya wa jimbo katoliki la Eldoret,Askofu Dominic Kimengich hii leo ameongoza misa yake ya kwanza katika kanisa la Moyo mtakatifu wa Yesu kathedrali.

Askofu amepokelewa na viongozi pamoja na wakristu kutoka madhehebu mbalimbali nje na ndani ya jimbo.

Misa hii imeandaliwa siku moja tu baada ya kusimikwa rasmi kwa askofu huyu katika sherehe ya kipekee iliyofanyika katika uwanja wa mama wa mitume seminari mjini Eldoret iliyohudhuriwa na maelfu ya waumini.

Sherehe hiyo ilianza rasmi na misa ambayo iliongozwa kwa sala fupi kutoka kwa mwadhama kadinali Yohane Njue kabla ya askofu Dominic kimengich Kubusu msalaba, kukariri kanuni ya imani, na kuketishwa katika kiti chake rasmi almaarifu kathedra.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *