Mahakama imetenga Jumatatu siku ya kuskizwa kesi iliyowasilishwa na gavana aliyetimuliwa Kiambu Ferdinard Waititu akipinga kubanduliwa kwake na seneti
Waititu alifika kortini akitaka uamuzi huu kubatilishwa kwa madai sheria haikuzingatiwa kwenye mchakato mzima wa kumtimua.
Mahakama imetenga Jumatatu siku ya kuskizwa kesi hiyo. Awali uapisho wa James Nyoro kuchukau wadhfa wa gavana ulisitishwa kutokana na kile kilichodaiwa ni utata kuhusu sheria.