Makali ya Sheria

Mahakama ya Iten imemtoza mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 22 dhamana ya shilingi 150,000 au mthamini sawa na hicho kwa madai ya kujaribu kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka 6.

Hosea Biwott alikabiliwa na shtaka  kuwa mnamo tarehe 28/1/2020 mwendo wa saa moja usiku katika kijiji cha Koibarak kaunti ya Elgeyo Marakwet alijaribu kumtendea kitendo hicho msichana huyo  kinyume cha sheria.

Mwanamume huyo alikabiliwa na shtaka lingine tofauti ya kushika sehemu zake za siri msichana huyo kwa kupenda. Mbele ya hakimu mwandamizi Charles Kutwo, jamaa huyo alikana madai hayo huku kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa mnamo tarehe 12/2/2020 na kusikizwa tarehe 25/2/2020.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *