Vuta Nikuvute Jubilee

Uhusiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto unazidi kutokota huku wawili hao wakiendelea kudhihirisha mvutano wa uongozi baina yao hadharani.

Ruto amejibu kauli ya Rais ya wiki iliyopita kwamba hatakuwa akimtuma kuzindua au kukagua miradi ya maendeleo kwa madai ya kujihusisha katika siasa, kwa kusema kwamba ataendelea kuzuru maeneo mbalimbali nchini kukagua miradi ya serikali.

Aidha, Ruto amesisitiza kwamba mshahara anaolipwa ni ishara tosha kwamba anastahili kuwahudumia Wakenya bila kujali miegemeo ya kisiasa na kwamba hajaingilia utendakazi wa kiongozi yeyote huku akisema kwamba sharti aheshimiwe. Ikumbukwe Rais akizungumza kwenye Kaunti ya Nyandarua alitoa kauli iliyoashiria kumlenga Ruto akisema amekuwa akiwatuma viongozi kuikagua miradi ya maendeleo ila alipozuru maeneo hayo hakukuwa na  chochote cha kujivunia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *