Wazazi washauriwa kuwapa wanao mashauri mema

Wazazi wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwaelekeza watoto wao  kwa kuwapa mashauri mema wakati huu kuna ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

 Akiongea na kituo hiki askofu wa jimbo katoliki la eldoret dominik kimengich amesema  kuwa wazazi wanastahili kuongea na watoto wao kwa misingi ya kidini ili wajiepushe  na makundi ambayo yanaweza kuwapotosha wakati huu shule zinazidi kufungwa.

 Amewahimiza wazazi kuwa waungane na watoto wao  kwa maombi wakati huu kila mtu anapitia hali ngumu ya maisha .

  Hata hivyo  amewatia  moyo wanafunzi   kuwa wawe wenye matumaini wakifuata mashauri na kuwa imani    siku zote kwa vile watakuwa washindi baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *