Hofu ya kudidimia kwa Korongo

Wanamazingira pamoja na walinda mazingira nchini walisema kuwa kuna haja kwa umma kuhamasishwa kuhusu hatari za ukataji misitu kiholela na kuharibu mazingira kwani hali hiyo imesababisha kupunugua kwa baadhi ya vizazi vya Wanyama na ndege msituni.

Kwa mujibu wa Maafisa kutoka huduma za wanyama pori nchini  wakiongozwa na afisa msimamizi wa ndege aina ya Korongo [CRANE BIRDS] Dkt. Mwangi Joseph ambaye alisema kuwa ndege hao wako kwenye hatari ya kudidimia kutokana na kupungua kwa idadi yao.

Aidha Maafisa hao wametoa wito kwa wakenya hasa wanaoishi katika sehemu za chemchemi vyanzo vya maji, kutunza mazingira sio tu kwa manufaa ya wanyama bali pia kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *