Monsinyo John Mbinda alitawazwa kuwa askofu wa nne wa jimbo katoliki la Lodwar siku ya Jumamosi tarehe nne
Mwakilishi wa Baba mtakatifu nchini na Sudan Kusini Mathews Herbatus Van Megen ametoa wito kwa askofu Mbinda kuwa mnyenyekevu katika utendakazi wake kama mchungaji wa jimbo hilo akiwaunganisha jamii jinsi roho mtakatifu alivyowaunganisha mitume wa yesu kristu alipowashukia siku ya pentekoste
Askofu Mbinda aliteuliwa na Baba mtakatifu mwezi wa February mwaka huu baada ya askofu wa tatu wa jimbo hilo askofu Dominic Kimengich kuteuliwa kuliongoza jimbo katoliki la Eldoret.
Tangu kuteuliwa kwa askofu Kimengich kuliongoza jimbo katoliki la Eldoret jimbo hilo katoliki la Lodwar limesalia chini ya usimamizi wake hadi leo hii.