Idara zashinikizwa kufunganya virago

Baraza la Maimamu kaskazini mwa bonde la ufa limeelezea haja kwa wakuu wa idara upelelezi wa jinai DCI na uongozi wa mashtaka ya umma DPP kusitisha migogoro uliopo baina yao na kuhangazia kutatua kesi za wakenya.


Wakizungumza Mjini Eldoret viongozi hao walisema wamekerwa jinsi Wawili wao wanavyo lumbana na wakenya wanawategemea kuwatatulia kesi na iwapo wataendelea na kutoleana Cheche za maneno inamaanisha wakenya watakosa kupata kutendewa haki.


Wakiongozwa na mwenyekiti wao Sheikh Abubakar Bini walisema kwamba yastahili idara ya DCI na DPP kuwa imara na wasiwe wanaweka wazi tofauti zao mbele ya wakenya.

Viongozi hao walieleza kuwa ni jambo la aibu idara tajika na ambazo zaheshimiwa kuwa na hulka za kukoseana heshima ikizingatiwa kuwa wao pia ni viongozi ambao wakenya wanataraji kuiga mfano wao kutokana na uongozi wao.

Kadhalika waliwasuta wanga’tuka mamlakani iwapo hawatoridhia kubadilisha mienendeo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *