KONGAMANO LA EKARISTIA ELDORET

Jimbo katoliki la Eldoret limeandaa kongamano la kwanza la Ekaristia takatifu lengo likiwa ni kuombea amani na kumbukumbu ya mtawa Anna Ali.

Kongamano hilo lilianza rasmi siku ya Jumanne katika kanisa la moyo mtakatifu wa Yesu kathedrali kwa misa takatifu huku mahujaji pamoja na wakristu wakianza hija yao hadi katika parokia ya Mtakatifu Patrick Burnt Forest ambako kutakuwa na kilele cha kongamano hilo siku ya Alhamisi.

Akihubiri katika misa hiyo askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ametoa wito kwa wakristu kuliombea amani haswa katika eneo la bonde la Kerio ambako kuna utovu wa usalama na kuliombea taifa ili nkuwepo na amani kuelekea uchaguzi mkuu Agosti tisa.

Askofu Kimengich kadhalika amemkumbuka mtawa Anna Ali aliyekuwa rafiki wa Ekaristia akisema kuwa alikuwa kielelezo chema jimboni hasa kwa kuabudiwa kwa Ekaristia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *