Askofu wa Jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amewataka wakenya kuliombea taifa hili liweze kuwa na amani uchaguzi mkuu ujao wa agosti 9 unapowadia.
Akiongea katika kanisa la St.Patriki Burnt-Forest katika Kaunti ya Uasin Gishu,Askofu amewashauri wakenya kuwa watu wa kuishi kwa amani na kama ndugu wala wasije wakatenganishwa kwa sababu za tofauti zao za kisiasa au hata kitabaka.
Askofu kimengich amewataka wananchi kujitenga na maswala ya ukabila ndipo taifa liweze kukua kimaendeleo akiwakumbusha wenyeji kuwa madhara yanayosababishwa na vurugu hasa wakati wa uchaguzu swala ambalo ametaja kuwa linavunja moyo kushuhudia wakenya wakizozana kwa sababu ambazo hazina msingi wowote.
Amewataka kuomba mungu aweze kuwakomboa na kumtegemea yeye wakati wote wa maisha yao na kwa hii huenda wakajiweka salama kwa kuishi na majirani zao kwa amani na mapendo.