WAENEZAJI CHUKI CHUMA CHAO KI MOTONI

wakaazi katika kaunti ya Uasin Gishu wameshauriwa kuwachagua viongozi wenye nia njema katika uongozi wala sio wale ambao wanaendeleza kampeni za ukabila na chuki.

kwenye mkao na wahabari katika makao makuu ya serikali ya kaunti mjini Eldoret,naibu gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Daniel Chemno amewataka wakaazi kuwa waangalifu na viongozi ambao wanawaingiza madarakani wasije wakajutia kwa kuwachagua wachochezi na viongozi wabinafsi.

wakati huo amekashifu baadhi ya viongozi kwenye ngazi ya kaunti wanaeneza chuki miongoni mwa wenyeji akisema kuwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

ameeleza kwamba viongozi walio mamlakani wakiongozwa na gavana Mandago wamekuwa mstari wa mbele kuhubiri amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *