Viongozi wa makanisa kanda la kaskazini mwa bonde la ufa NCCK wamewahimiza wananchi kudumisha amani kabla,wakati na hata baada ya uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 9 mwaka huu.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao kasisi Daniel Barno wakizungumza mjini Eldoret,wamesema watahakikisha wenyeji wanadumisha amani uchaguzi huu na hata baada ya uchaguzi akiwashauri wakenya kuwa mabalozi wa amani.
Viongozi hao wamewasuta wanasiasa dhidi ya kueneza kampeni za chuki wakiwataka wauze sera zao kwa njia ya uwazi na wananchi watawachagua iwapo wataridhika nazo.
Kadhalika,viongozi hao wamewaomba wakenya kuvumiliana licha ya tofauti zao za vyama akiwakumbusha kuwa uchaguzi ni wa siku moja tu na utapita hivyo kuwashauri kuishi kwa amani na upendo.