TUNZA MAZINGIRA UWE HAI

Wakenya wameshauriwa kuwa mstari wa mbele kuyatunza mazingira kwa kuepukana na utupaji taka ovyo,kama njia moja ya kuhifadhi  mazingira.

Wakizungumza kwenye kongamano lilio waleta pamoja Washikadau na wanaharakati wa mazingira katika mji wa Eldoret,wanaharakati hao wamesisitiza haja ya wakenya kuungana kuyatunza mazingira kwa mafaao ya kizazi kijacho.

Wakiongozwa na Cliff Barkach mwakilishi wa mamlaka ya mazingira NEMA ,kuna sheria ambayo inastahili utekelezaji wake ili kuhakikisha kila mkenya anazingatia nafasi yake ya utunzaji mazingira iwe ya kutoa bidhaa au utumizi wake.

Mshikadau mwingine Nyakwach Obiero ,amedadisi kuwa baadhi ya bidhaa zinaweza kutumika hata zaidi na wanaendelea na mufundisho kwa wakenya kutambua suala hilo na kukabili uchafuzi wa mazingira.

Kwa upande wake, Bernad Kigen mwakilishi wa baraza linalosimamia idadi ya watu nchini amesema kwamba,watu wengi wamepata magonjwa yanayotokana na uchafu na ili kuhakikisha kwamba wanadhibiti magonjwa hayo, wataendelea kuwapa hamasisho wakenya na nanma wanaweza kuyatunza mazingira yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *