Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Maurice Muhatia Makumba ametoa wito kwa wakristu kuishi maisha ya sakramenti.
Akihubiri katika parokia ya St Zachaeus kajimbo askofu mkuu Muhatia aliwakumbusha wakristu kujelea desturi ya awali ambapo Kila mkristu alitakiwa siku ya jumamosi kabla ya Misa kwenda kwenye kitubio kama njia moja kujiandaa kwa ajili ya Misa siku ya Dominika.
Alitoa wito kwa wakristu kutunza amri za Mungu akisema kuwa ni mwongozo ambao huwapa wakristu ujasiri ya kupambana na misukosuko ya maisha