Maandalizi za Mbio za masafa marefu za Eldoret City awamu ya tano ambao imeratibwa kuandaliwa April 21 mwaka huu yamekamilika.
Kulingana na msimamizi wa mashindano hayo Moses Tanui ni kwamba zoei la kujiandikisha linakamilika kesho,kabla ya majina kamili kutolewa kabla ya hiyo siku.
Tanui alisema kwamba wananuia kuwashirikisha wale ambao wana nia ya kushiriki mbio hizo na hawana fedha kadhalika watashirikishwa na kupewa nafasi katika mbio hizo.
Msimamizi huyo alisema wamebadilisha barabara zitakazotumika kwa kuwa wengi wa wanariadha hawana makocha na kuwapunguzia mizigo na kero pa kuweka mizigo yao.
Ikumbukwe kuwa ,mbio za Eldoret City zilikua zimesitishwa kwa muda kutokana na wafadhili kusitisha msaada wao.