Padre Kirui; igeni Mama Bikira Maria

Wakristu wamehimizwa kuiga mfano wa Mama Bikira Maria kwa kuwa wapole na watiifu katika maisha yao.

Padre Charles Kirui kwenye homilia yake wakati wa Misa ya asubuhi katika kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Kathedrali, amewataka wakristu kutambua na kuheshimu jukumu kubwa la Mama Bikira Maria katika safari ya ukombozi wa wanadamu.

Wakati uo huo padre Kirui amesema kuwa mkristu hawezi kuchagua kumpenda Yesu na kumwacha mamake Bikira Maria kwani ndiye aliyekubali kuwa chombo cha Mungu katika safari ya ukombozi.

Kadhalika amewahimiza kina mama kujivunia wito wao wa kuwa wazazi kwani ni Baraka kubwa kutoka kwa Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *