Atwoli Kujumuika Rais Uhuru Kuhutubia Wakenya siku ya Labour Day

Rais Uhuru Kenyatta na katibu wa muungano wa wafanyikazi Francis Atwoli watahutubia Wakenya siku ya Leba Dei, Ijumaa Mei 1.

Atwoli alisema tayari ametuma mwaliko kwa Rais Uhuru ili ajiunge naye pamoja na viongozi wengine katika kuwahutubia Wakenya siku hiyo. Akiongea Alhamisi, Aprili 23, Atwoli alisema vyombo vya habari pia vimealikwa ili viweze kupeperusha habari kwa Wakenya.

Katibu huyo aliongeza kuwa ni Rais atachagua ukumbi ambapo mkutano wao utafanyika ili waweze kuwahutubia Wakenya.

Wafanyikazi wamekuwa na masaibu mengi tangu janga la coronavirus liingie humu nchini na kuathiri shughuli nyingi kiuchumi. Mamia ya wafanyikazi walitumwa nyumbani katika likizo ya lazima bila malipo huku wengine wakipunguziwa mshahara wao.

Kupata riziki pamoja na kodi ndio yamekuwa matatizo makubwa zaidi kwa wafanyikazi haswa wanaotegemea malipo ya chini. Akiongea kwenye Ikulu Jumatano, Aprili 22, Rais Uhuru alivunja matumaini ya wengi baada ya kusema kuwa hana uwezo wa kuagiza ulipaji wa kodi kusitishwa. Alisema nyumba ni mali ya watu binafsi na serikali haiwezi kuingilia hilo ila tu wapangaji wasikizane na wenye nyumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *