Mataifa mengi barani Afrika yameanzisha utaratibu wa kupiga marufuku ya kutotoka nje ikiwa ni jitihada ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.
Lakini je, watu wenyewe wanahusishwa katika maamuzi haya kama yanaweza kufanyika kwao?
Mataifa ya barani Afrika yamejifunza namna ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama maambukizi ya virusi vya Ukimwi na Ebola hivyo wanaweza kutumia uzoefu huo kukabiliana na madhara ya ugonjwa wa Covid-19.
Jambo muhimu ambalo jamii inapaswa kujifunza ni kutorudi nyuma katika mapambano ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
Huu ndio uhalisia wa maisha.
Kwanza, mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza huwa unakuja kitofauti katika jamii mbalimbali, kwa mujibu wa hali za watu husika wa eneo husika.
Jambo lingine ni hatua za kukabiliana na janga lenyewe kwa mfano amri ya kuzuia watu kutoka nje, inaweza kuchukuliwa bila watu kuridhia matokeo yake.
Ni pale tu wananchi wenyewe wanaposhirikishwa katika mipango na utekelezaji wake wa kukabiliana na mlipuko huo, ndio jitihada zinaweza kufanikiwa.