Washukiwa sita wanazuiliwa katika kituo cha elbergon kaunti ya nakuru kwa tuhuma za kuhusika katika unajisi wa mwanamke wa miaka 45 .
Kulingana na chifu wa eneo hilo Jonah komen watuhumiwa waliokolewa kutoka mikononi mwa umati uliotaka kuwaangamiza.
Mumewe mwaathiriwa amedokeza kuwafahamu baadhi ya wahusika huku mkewe aliyetendewa unyama huo akitibiwa katika hospitali ya elbergon na kuruhusiwa kwenda nyumbani.