wito umetolewa kwa waumini wa kanisa katoliki na wakenya kwa ujumla kuwaombea waathiriwa wa virusi vya corona pamoja na wauuguzi wanaowahudumia wahanga hao.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa runinga ya mtandao ya kanisa la katoliki nchini almaarufu Ukweli Tv mwenyekiti wa idara ya mawasiliano katika baraza la maaskofu nchini KCCB askofu Joseph Obanyi ametoa wito kwa wakenya kwa ujumla kuzingatia maagizo yaliyotolewa na serikali ili kuepuka maambukizi zaidi ya virusi vya corona.
Askofu Kadhalika ametoa wito kwa vyombo vya habari na wale wanaotaoa habari potovu kupitia mitandao yao kukoma kufanya hivyo na badala yake kutumia vyombo hivyo na mitandao kueneza habari za matumaini hasa wakati huu ambapo taifa linapambana na ugonjwa wa covid 19.