Mataifa ya Tanzania na Somalia yamekuwa matifa ya hivi punde kurekodi visa vya kwanza vya maambukiza ya virusi vya corona
Mnamo hio jana, msafiri huyo aliiingia Tanzania majira ya saa kumi jioni. Mgonjwa huyo aliyetangazwa ni mwanamke wa miaka 46 raia wa Tanzania, ambaye aliwasili kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la Rwanda.
Msafiri huyo aliondoka nchini tarehe 3, Machi 2020 ambapo kati ya tarehe 5-13 Machi alitembelea nchi za Sweden na Denmark na kurudi tena Ubelgiji. Msafiri huyo alipita uwanja wa ndege wa KIA.
Waziri Ummy Mwalimu amesema msafiri huyo alipofika KIA alifanyiwa ukaguzi na maafisa wa afya na kuonekana kutokuwa na homa.