Serikali ya Kaunti ya Elgeiyo Marakwet Yasitisha Biashara

Serikali ya kaunti ya Elgeyo Marakwet imesimamisha biashara zinazoendelea katika kaunti hiyo kwa muda wa siku 30 kama njia moja kukabiliana na virusi vya korona.

Akiongea na wanahabari baada ya mkutano uliowaleta pamoja kamati ya dharura na maafisa wa afya, Tolgos amesema kuwa biashara ya  mnada ,soko za kila wiki, vyumba vya burudani , biashara ya uchuuzi na kambi ya wanariadha.

Tolgos vile vile ametaka  maji safi na sabuni ya kunawa mikono kuwekwa katika ofisi zote zinazotoa huduma kwa wananchi na vituo mbali mbali vya kuegeza magari

Hata hivyo amewasuhi watakahitaji huduma katika ofisi za serikali ya kaunti hiyo kutumia njia mbadala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *