Wahudumu wawili wa pikipiki na abiria mmoja wameripotiwa kufariki usiku wa kuamkia leo baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabara katika barabara ya Iten Kabarnet.
Inaaminika kuwa wahudumu hawa walikuwa wakiendesha pikipiki kwa mwendo wa kasi kabla ya kukongana ana kwa ana katika eneo la Kessup.
Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi katika kaunti ya Elgeyo Marakwet John Mwinzi amesema kuwa mmoja wao alifariki papo hapo huku mwingine akiaga alipokuwa akipelekwa hospitali na mwingine akipoteza maisha yake alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa mjini Iten.