Waumini wa kanisa katoliki kote ulimwenguni hii leo wameadhimisha Jumatano ya majivu ikiashiria mwanzo wa kipindi cha kwaresma sambamba na kampeni yenye maudhui ya “Uongozi Bora unaobadilisha taifa, wajibu wangu”.
Wakristu wa jimbo katoliki la Eldoret hii leo wameungana na wakristu wengine duniani ili kuanza rasmi kipindi cha kwaresma kitakacho dumu kwa siku arobaini.
Kila mwaka kanisa Katoliki nchini kupitia tume ya haki na Amani (CJPC) huzindua kampeni ya Kwaresma yenye mada maalum ambayo huanza baada ya Jumatano ya Majivu.
Maudhui ya mwaka huu ni “Uongozi Bora unaobadilisha Taifa, Wajibu wangu”.
Akizungumza na kituo hiki afisini mwake, askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich, amewarai wakristu kuzingatia maelekezo na mafunzo kwenye nakala maalum kwa ajili ya kipindi hiki muhimu.