Seneta wa Narok Ledama Ole Kina amekamatwa na maafisa wa tume ya uwiano na utangamano nchini-NCIC kufuatia matamshi ya uchochezi mwishoni mwa wiki jana.
Ledama amekamatwa nje ya afisi za kampuni ya Royal Media jijini Nairobi.
Seneta huyo anatarajiwa kuandikisha taarifa kuhusu matamshi anayodaiwa kutoa wakati mkutano wa kupigia debe mchakato wa BBI katika kaunti ya Narok. Hapo jana baadhi ya viongozi eneo la North Rift walikashifu vikali matamshi ya Ole Kina wakiyataja kama yanayonuia kusababisha uhasama wa kijamii na kuahidi kupinga mikutano ya BBI ikiwa italeta migawanyiko baina ya wakenya.