Matakaa ya Paspoti sasa ni Mwaka Moja

Serikali imeongeza makataa kwa wakenya wanao saka pasporti mpya hadi mwaka mmoja

Katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiang’i walio na paspoti hiyo wana hadi tarehe mosi mwezi machi mwaka ujao kabla ya kuwacha kutumika rasmi

Amelalamikia idadi ya wakenya walio ugaibuni ambao hawajabadilisha pasporti zao akisema kwa sasa wako takriban milioni moja nukta nane. Matiang’i amesema ili kurahisisha kupata huduma hiyo serikali imebuni vituo katika kaunti za Nakuru, Uasin Gishu, Embu na Kisii huku zingine zikibuniwa katika miji ya Berlin, London, Paris, Washington DC, Johannesburg  na Dubai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *