Roho mtakatifu mwanga wa amani na matumaini

Askofu wa jimbo katoliki la Murang’a askofu James Maria Wainaina mapema hii leo amewaongoza wakristu kote nchini, katika misa takatifu ya  kuadhimisha sherehe ya pentekoste katika kanisa la Holy Family Basilica jijini Nairobi.

Katika homilia yake askofu Wainaina, amewakumbusha wakristu kuwa kupitia roho mtakatifu, yesu kristu anaendela kuisha ndani ya kanisa na kuendeleza kazi ya wokovu.

Askofu pia ameelezea kuwa ni vigumu kuelewa mambo ya kiroho ambayo ni  fumbo na hivyo basi mkristu anahitaji roho mtakatifu ili kumsaidia kuyachambua mafumbo hayo ya imani ambayo yamefichika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *