Kaunti hii ya Uasin Gishu imeingia kwenye orodha ya kaunti ambazo zinapepetwa na janga la virusi vya corona, baada ya kuandikisha visa kumi na moja vya maambukizi ya virusi vya Corona hadi kufikia sasa.
Katika kikao na wanahabari hii leo katibu mwandamizi katika wizara ya afya Rashid Aman amesema kuwa kumi na moja hao wanatoka katika eneo la Turbo, huku zoezi la kuwatafuta waliotangamana na waathiriwa hao likiendelea.
Katibu huyo kadhalika amesema kuwa chini ya saa ishirini na nne baada ya kufanya sampuli kwa watu elfu mbili mia tisa hamsini na tisa, Kenya imesajili visa mia moja arobaini na tatu vya virusi vya corona na hivyo kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa elfu moja mia nane themanini na nane.
Aman amesema kuwa kati ya visa hivyo vipya idadi ya wanaume ni mia moja na kumi wan awake wakiwa thelathini na tatu umri wao ukiwa kati ya mwezi moja na miaka themanini na nane.