Kenya yapongezwa kwenye vita dhidi ya COVID-19

Kenya imepongezwa kutokana na juhudi zake zake za kukabili kuenea kwa virusi vya Corona kufikia sasa.

Kwenye mahojiano ya kipekee kwa njia ya simu na kituo hiki, balozi wa Marekani humu nchini Kyle McCater, amesema Kenya inafaa kujivunia kuwa na wataalam wa ngazi ya juu katika masuala ya utafiti kuhusu chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali, kadhalika utayarifu wake kuhusu janga la Corona.

Wakati uo huo McCater ameishauri serikali kutolegeza kamba katika juhudi zake za kukabiliana na magonjwa mengine sugu kama vile Malaria, Kifua kikuu na Virusi vya Ukimwi wakati huu wa janga la Corona.

Amesema ni vyema wananchi kuendelea kupata huduma za matibabu kutokana na magonjwa mengine kwani huenda yakasababisha vifo zaidi kuliko virusi vya Corona ikiwa wananchi wataoogopa kutembelea vituo vya afya.

Kuhusu wazo la serikali kulegeza baadhi ya masharti dhidi ya Corona ili kufungua uchumi wake, balozi huyo amesema hatua hiyo itategemea pakubwa tabia za wananchi za kuendelea kufuata maagizo wakati wa kurejelea shughuli zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *