Ebola haujaenea Kenya asema Duale

Waziri wa afya nchini Aden Duale amewaondolea hofu wakenya kuhusu ugonjwa wa Ebola akisema haujaenea nchini.

Duale amesema licha ya kuripotiwa kisa cha kwanza nchini, ni kisa kilichotoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kwamba wakenya hawafai kuingiwa na hofu.

Kulingana naye, serikali imekuwa ikiweka mikakati tangu ugonjwa huo kuripotiwa nchini DRC na juhudi zaidi zinaendelea kuwekwa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Watu 57 waliotangamana na mgonjwa huyo wamebainishwa na wanafuatiliwa huku serikali ikiimarisha uchunguzi katika vituo vya kuingilia humu nchini.

Serikali pia imesema sampuli 268 zimepimwa ambapo moja imebainika kuwa na Ebola. Waziri Duale amewahakikishia wananchi  na jumuiya ya kimataifa kwamba Kenya bado ni salama kwa safari, Utalii na biashara huku akisema serikali itaendelea kuchukua hatua zote hitajika ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *