Kamishna wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet David Koskei, ametoa onyo kali kwa wakazi wanaoishi nyanda za juu za bonde dhidi ya kuchoma mimea wanapoandaa mashamba yao kwa kilimo, akitaja hatua hiyo kama mojawapo ya vyanzo vya maporomoko ya ardhi yanayoikumba kaunti hiyo mara kwa mara.
Mwakilishi wa shirika la msalaba mwekundu eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa, Oscar Okumu amewataka wakazi kuchukua tahadhari za mapema kutokana na mvua kubwa zinazotarajiwa katika msimu wa Oktoba hadi Desemba mwaka huu.
Okumu amesema baadhi ya maeneo yametambuliwa kuwa hatari ya kukumbwa na mafuriko huku pia akiwataka wakazi kuepuka kuvuka mito iliyofurika maji.
Hayo yakijiri, mkurugenzi wa mawasilinao katika afisi ya gavana wa Uasin Gishu Sila Kosgei, amewataka wakulima kutumia mvua hizo kukuza mimea inayokomaa kwa muda mfupi.
