Ikiwa imesalia juma moja kanisa katoliki kuadimisha jumapili ya matawi,kanisa bado linasubiria maagizo kutoka kwa serikali kuhusu sheria zilizowekwa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.
Kama ilivyo ada,wakristu hukongamana kuadimisha siku kuu hii,kila mwaka wa kalenda ya kanisa,lakini kulingana na askofu wa jimbo katoliki la Eldoret,askofu Dominic Kimengich,huenda mwaka huu ikawa na mabadiliko ikizingatia changamoto ambalo taifa linazidi kukumbana nayo ya virusi vya covid-19.