Uhispania sasa limekuwa taifa la pili kuongoza kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya Corona duniani.
Idadi ya vifo imeongezeka kwa watu 738 ndani ya saa 24 kila siku na kufanya idadi ya vifo hivyo mpaka sasa kufikia 3,434, idadi ambayo iko juu zaidi ya Italia.
Ukilinganisha taarifa rasmi za China ambazo ziliripoti vifo 3,285 huku nchi ambayo imeathirika zaidi duniani, Italia ikiwa na vifo 6,820. Idadi ya maambukizi Uhispania imeongezeka mara tano na karibu watu 27,000 wanatibiwa kila siku hospitalini.
Pamoja na makatazo mengi duniani bado virusi vya corona vinaonekana kuwa changamoto kubwa duniani, mpaka sasa dunia ina wagonjwa 478,331 na vifo zaidi ya 21,524 huku watu zaidi ya 114,832 wamepona ugonjwa huo kwa mujibu takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins .
Wakati huohuo Marekani ikiwa kwenye hali tete ambapo visa 70,000 vya virusi vya corona vimethibitishwa na vifo vyapatavyo 1,050. Idadi ya maambukizi imeonekana kuongezeka kwa zaidi ya 10,000 kwa siku moja.
Ingawa si habari mbaya tu imepatikana kwa Marekani, kwa sababu gavana wa New York amesema kuwa hatua za makatazo yaliyowekwa yameanza kutekelezwa kikamilifu na matokeo wameanza kuyaona. Huku China katika jimbo la Hubei, ambako maambukizi ya virusi hivi vya corona vilianzia hali ikiwa shwari na hakuna maambukizi mapya yaliyoripotiwa.
Hatahivyo idadi kubwa ya maambukizi kutoka China imeripotiwa. Kwa upande wa Uingereza vifo vimeongezeka na kufikia 463 awali vilikuwa 422, wakati maambukizi ya ugonjwa huo yakiwa zaidi ya 9,500.