Viongozi wa dini la Kiislamu Ukanda wa North Rift, wamepongeza hatua ya Rais William Ruto kutaka kufanya mazungumzo baina yake wakenya pamoja na viongozi mbalimbali wakisema ni hatua ya kufana kwa uwiano wa kitaifa.
Wakizungumza mjini Eldoret,viongozi hao walisema kwamba mazungumzo hayo yaweze kuwa yenye mwelekeo wa kitaifa na si wa kibinfasi.
Viongozi hao wakiongozwa na Sheikh Abubakar Bini wanapendekeza, viongozi watakaoshiriki mazungumzo hayo wasitishi misimamo mikali kwa manufaa ya taifa.
Viongozi hao walitumia fursa hiyo kusisitiza uwezekano wa kuimarika kwa shughuli za maabadi ,kwa kusitishwa kwa wanasiasa kuhusishwa kwenye michango ya harambee kwenye maeneo ya ibada,wakieleza kwamba ilikua inatumiwa vibaya na wanasiasa kuwalaghai wakenya.