Kanisa la ACK ukanda wa Northrift limetoa wito kwa wazazi kuzungumza na wanao kwa kina likisema kuwa visa vinavyoshuhudiwa kwa sasa nchini huenda ikawa ishara ya utovu wa nidhamu miongoni mwao.
Likiongozwa na askofu wa Eldoret Chrisptopher Ruto kanisa hilo limesema kuwa matokeo nay ale yaliyoshuhudiwa katika maandamano yaliyoongozwa na vijana wa kupinga mswada wa kifedha wa mwaka 2024 ni ishara tosha kuwa wazazi wengi wamefeli katika malezi wakitoa wito kwa kila mzazi kuanza mchakato wa kuwarudi wanao.
Wametoa wito kwa kanisa kusimama kidete kushirikiana na wazazi katika kudumisha nidhamu miongoni mwa vijana wakitoa wito kwa vijana kadhalika kukubali kusikiliza wale walio na umri kuwazidi.