Kenya yangu,kenya yako

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB limeandaa kikao na rais William Ruto katika ikulu jijini Nairobi.

Baraza hilo likiongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Maurice Muhatia Makumba lemesema kuwa lengo la mkutano huo ni kutafuta suluhu kwa maswala ambayo kwa sasa yamewasakama wakenya yakiwemo maandamano yaliyoshuhudiwa hivi majuzi ya kupinga mswada wa kifedha wa mwaka wa 2024.

Kwenye mtandao wa kijamii ya X ikulu ya rais imeshabikia ushirikiano baina ya serikali na baraza hilo ikisema kuwa hii ni njia mojawapo ya kutafuta suluhu kwa changamoto mblimbli za kitaifa.

Haya yanajiri wakati ambapo kuna kampeni kwenye mitandao ya kijamii ambapo viongozi wa kidini wanashinikizwa kutojihusisha na wanasiasa swala wanalo sema kuwa kanisa linaonekana kutekwa nyara na wanasiasa hao wakiebdesha kampeni ya clean the alter.

Wanaharakati hao sasa wameanzisha mchakato wa kuwatumia ujumbe viongozi mbalimbali wa kidini wakiwashawishi kukoma kujihusisha na wanasiasa na badala yake waangazie maswala ya kidini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *