Kungatuka kwetu mtalionea mwezi

Jamii ya Ogiek katika eneo la Sasamwani katika msitu wa Maasai Mau kaunti ya  Narok wameitaka serikali kuheshimu uamuzi wa mahakama na kuwapa hati miliki.

Wakizungumza mjini Narok wakiongozwa na mwenyekiti wa wao Wilson Memusi,alisema jamii yao ilifurushwa kwenye msitu huo mwaka jana bila notisi.

Memusi alisema walipewa ardhi hiyo mwaka wa 1975, baada ya kushinda kesi kwenye mahakama ya kimataifa nchini Arusha Tanzania.

Aidha,alisema kwamba ardhi takriban ekari tatu inayosemekana kutengwa kuwapa ridhaa waliofurushwa msituni humo, haijawajumuisha watu kutoka jamii ya Ogiek.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *