Monsinyori Peter Munguti Makau anatarajiwa kupewa daraja la uaskofu kama askofu mwandamizi wa jimbo katoliki la Isiolo.
Sherehe hii ambayo itaongozwa na balozi wa Baba Mtakatifu nchini Mathews Hurbetus Marian Van Megen miongoni mwa maaskofu wengine nchini itaandaliwa tarehe ishirini na saba mwezi huu katika jimbo hilo.
Monsinyori Peter Makau alitoa wito kwa wakristu wenye nia njema kuendelea kuombea jimbo hilo ambalo linatarajiwa kuwa na hafla ya kihistoria mwaka moja tu baada ya kupandishwa hadhi na kuwa jimbo.
Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na askofu wa kwanza Antony ireri Mukobo wa shirika la Consolata ambaye amekuwa vikari wa Vikarieti ya Isiolo kwa kipindi kirefu. Ikumbukwe kuwa Monsinyori Peter Makau atakuwa askofu wa pili wa jimbo hilo baada ya jimbo hilo kukwezwa baada ya kuwa Vikarieti kwa muda wa miaka ishirini na tano chini ya Vikari Antonio Ireri Mukobo ambaye kwa sasa anatazamiwa kustaafu.