Wakristu wamehimizwa kujisadaka bila kujibakisha kwa umarishaji wa imani yao.
Akihubiri katika kanisa la Mathari ,Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria amesisitiza haja ya wakristu kuishi maisha yanayompendeza mwenyezi mungu na kujitenga na majivuno.
Alisema kwamba, baadhi ya wakristu huvunja mkataba na kristu kwa kujihusisha na maswala ambayo hayastahili na sio ya kiutu,akiwaeleza kwamba lengo la ukristu ni kujijenga kiimani,kando na kuwa mfano mwema kwa wale ambao hawajamfahamu huyo kristu.
Vilevile,askofu mkuu aliwataka wakristu kuwa hulka ya kuwasamehe wengine akieleza kuwa wanadamu wamejawa na mapungufu na kila muda anaweza akakosea.
Askofu mkuu Muheria alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kuhakikisha kwamba wanajipatia bima ya Afya ya umma ili wanapotafuta huduma ,wasije wakashindwa kugharamia matibabu ya mgonjwa wao,akiongeza kwamba,bima hiyo upunguzia jamii mzigo mzito wakati wa matibabu hasa magonjwa sugu.