Hongera mkuu wewe ndiye bazuu

Mashirika mbalimbali ya kijamii katika kaunti ya Uasin Gishu wameendelea kupokeza hatua alizochukua rais William Ruto ya kuvunjilia mbali baraza lake la mawaziri wakisema ni hatua ya kupigiwa mfano.

Wakiongozwa na afisa mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Center For Human Rights and Democracy Kipkorir Ng’etich ni kwamba,ni jukumu sasa la Rais kutathmini ni mawaziri wepi ambao atawapa nafasi hiyo kwa kuzingatia matakwa ya mwananchi.

Afisa huyo vilevile alisema mwelekeo ambao serikali ilikua inaelekea haikua inaridhisha na kauli aliyokata rais huenda ikasaidia taifa kuelekea ukwamuaji wa uchumi wa nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *