Askofu wa msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Simon Peter kamomoe amesema kuwa ukosefu wa uchaji wa Mungu umechangia masaibu mengi ambayo taifa la Kenya linapitia kwa sasa.
Akizungumza katika misa ya kuwazawadi wanafunzi wa shule ya Holy Innocence Taasia jimbo kuu katoliki la Nairobi askofu Kamomoe alisema kuwa hali inayoshuhudiwa nchini yakiwemo ufisadi umechangiwa na ukosefu wa kumtegemea mwenyezi Mungu.
Alisema kuwa swala la uwajibikaji linastahili kukuzwa kutoka katika ngazi ya familia kwa faida ya taifa bora katika siku zijazo.
Alitoa wito kwa kila mmoja kujiepusha na ufisadi akisema kuwa ufisadi ni dhambi ya mauti ambayo itamnyima mja kukutana na muumba wake.
Askofu Kamomoe alitoa wito kwa wazazi kuwafunza wanao mila zilizo njema na siku zote kuwa mfano bora wa kuigwa.